![]() |
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Ya Dar es salaam,Simon Sirro |
Watu wasiojulikana
wamevamia na kuvunja ofisi ya kamishna Mkuu wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kuiba kompyuta
na vifaa vingine.
Habari tulizozipata ambazo
zimethibitishwa na Polisi kanda maalumu ya Dar es
Salaam zinasema miongoni mwa kompyuta zilizoibiwa ni ile
iliyokuwa inatumiwa na Dr Philip Mpango alipokaimu
nafasi ya Kamishna mkuu wa TRA kabla ya kuteuliwa kuwa
Waziri wa Fedha
Kwa mujibu wa chanzo hicho,huenda
kompyuta hiyo ikawa na taarifa muhimu kuhusu ukwepaji wa kodi na
sakata la makontena Bandarini.
Kamanda wa Polisi Kanda
Maalumu Ya Dar es salaam,Simon Sirro amesema tayari jeshi hilo
linawashikilia watu wanne kwa uchunguzi zaidi
Siro alitaja vitu
vilivyoibwa katika ofisi hiyo kuwa ni
Kompyuta mbili, Televisheni moja na King'amuzi.
Alisema wanaoshikiliwa
ni walinzi wawili kutoka kampuni ya Suma
JKT ambao walikuwa zamu usiku huo, Katibu Muhtasi
pamoja na Karani wa Ofisi hiyo.
Tangu aingie madarakani, Rais John Magufuli amefanya mabadiliko katika mamlaka hiyo kwa kumwondoa aliyekuwa Kamishna Mkuu, Rished Bade na kumteua Dk Mpango kukaimu nafasi hiyo, kabla ya kumteua kuwa Waziri wa Fedha na nafasi hiyo kuchukuliwa na Alphayo Kidata.
Katika kipindi hicho, baadhi ya wafanyakazi wamewajibishwa kwa kusimamishwa kazi kutokana na tuhuma za ama kushindwa kusimamia vyema ukusanyaji wa mapato au kushirikiana na wafanyabiashara kukwepa kodi na kulisababishia hasara Taifa.

0 comments:
Post a Comment