Habari Mpya

Friday, February 13, 2015

LOYAL MEDIA BLOGSPOT NDANI YA MOSJOSO

wanafunzi wa chuo kikuu cha Mzumbe kozi ya Utawala na Utunzaji kumbukumbu stashahada mwaka wa kwanza  kushoto ni Mwahija Kisomi na Dominicus Nyoni kulia kutoka kikundi cha The Loyalmedia.blogspot.com wakisikiliza maelezo kutoka kwa Rais wa Serikali ya wanafunzi ya Chuo cha Uandishi wa Habari Morogoro (MOSJOSO) Kelvin Philipo hayupo pichani


   Kikundi cha The  Loyalmedia.blogspot.com kutoka   chuo kikuu cha Mzumbe wametembelea chuo cha Uandishi wa Habari Morogoro MSJ kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu tasnia ya habari.

   Akitoa maelezo katika chumba cha mikutano chuoni hapo raisi wa serikali ya wanafunzi MSJ MOSJOSO Kelvin philipo amesema kuwa amefurahishwa na ugeni huo kwani ushirikiano ambao ulikuwa ukifikiriwa kwa maneno na umeanza kwa vitendo.

   “niseme nimefurahishwa sana na ujio wenu kutokana na mara kwa mara kutafakari juu ya ushirikiano wetu na Mzumbe kwani sisi tunaonekana kujifunza vitu tofauti hivyo niseme nafurahishwa sana na haya ninayoyaona kwa sasa hivyo karibuni sana’. Alisema Kelvin.

    Naye waziri wa habari chuoni hapo Timotheo Lupembe amesema kuwa wanajivunia kuona mzumbe wamewapa kipaumbele kuja kujifunza masuala ya habari kitu ambacho kitawafanya waungane kwa pamoja katika kujenga nchi yetu.

  Kikundi hiko kinajihusisha na utoaji wa habari kwa njia mtandao wa kijamii blogs kinahusika kusambaza picha na habari zinazohusu chuo cha Mzumbe ili kuwahabarisha na kuwaburudisha wasomaji wao.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: LOYAL MEDIA BLOGSPOT NDANI YA MOSJOSO Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top