DAWA MPYA YA KUTIBU MAJI MACHAFU YAGUNDULIKA :
Edited by Godfrey Mgallah.
Kampuni ya Warioba Sanitation inayoshughulika na
uchunguzi wa dawa za kutibu maji Mkoani Morogogo yagundua dawa mpya ya kutibu
maji machafu.
Dawa hiyo inayotambulika kwa jina la MSELE WATER
GUARD ambayo imedhibitiswa na mkemia mkuu wa kampuni hiyo Warioba Igombe na
kusema “Dawa hii inauwezo wa kutibu maji machafu ambayo yatakuwa yana rangi
mbalimbali na kusababisha kuwa meupe kwa muda mfupi”
Hata hivyo mkemia ameongeza na kusema dawa hii
nimaarumu kwa mikoa yenye ukame kwani hutumia maji yaliyo kwenye madimwi,
mabwawa hivyo basi dawa hii itawasaidia katika usafishaji wa maji yao.
END
KOZI FUPI YA UTANGAZAJI YAANZISWA:
Edited by Nasibu Babisha.
Chuo Cha Uandishi wa Habari Morogoro (MSJ)
kimetangaza kozi mpya ya utangazaji wa Tv na Radio chuoni hapo.
Akiongea na MOSJOSO blog msemaji mkuu wa chuo hicho
Michael Sikapundwa amesema kuwa kozi hiyo itaanza mwezi wa kwanza mwaka kesho.
Msemaji huyo aliongeza kwa kusema kuwa kozi hiyo
itachukua muda wa mwezi sita kwa gharama ya shilingi laki nne kwa kozi hiyo.
Hatahivyo Mratibu wa mafunzo wa Chuo Cha Uandishi wa
Habari Morogoro Godfley Marusu ameongeza kwa kusema “wazo la kuongeza kozi hiyo
katika Chuo hicho ni ni kuongeza wataaramu katika tasnia ya uandishi wa habari
kwani kuna upungufu mkubwa katika taaluma hiyo”.
END
MZALENDO COMPANY YAANZISHA KOZI MPYA YA KOMPUTA:
Edited by Godfrey Mgallah.
Kampuni ya Mzalendo iliyopo Kihonda Mkoani Morogoro
Imetangaza kozi mpya ya Adobe Page Maker ambayo inahusika na utengenezaji wa
vitabu, magazeti, majarida, vipeperushi na hata kadi za mialiko.
Akizungumza na MOSJOSO blog Msemaji Mkuu wa kampuni hiyo
Frank Bruno amesema kuwa “kozi hii mpya itasomwa kwa miezi mitatu na kuhitimu”.
Aidha aliongeza kwa kusema “kozi hii itamuwazesha
mwanafunzi kuajiriwa au kujiajili mwenyewe ili kuendana na soko la ajira nchini”.
Hatahivyo msemaji huyo aliongeza kwa kusema kuwa “mwanafunzi
atakaye hitaji kusoma kozi hii atapata fursa ya kusoma bure kozi ya awali ya
komputa (introduction of computer).
END
BIDHAA MPYA YA MAZIWA FRESH YAZINDULIWA MOROGORO:
Edited by nasibu babisha.
Kampuni inayojishughulisha na usindikaji wa maziwa
ya Jogosha Milk ya mkoa morogoro imezindua bidhaa yake mpya yenye ujazo wa
mililita 300 inayofamika kwa jina la Jogosha Fresh Milk.
Akizungumza na MOSJOSO blog msemaji mkuu wa kampuni
hiyo Godfrey Mgallah amesema “bidhaa yetu mpya itasaidia kuimarisha mifupa,
ngozi na kupunguza kiasi cha sukari mwilini kwa watumiaji wa bidhaa zetu”.
Hatahivyo msemaji huyo ameongeza kwa kusema Jogoha
Fresh Milk inapatikana kwa bei za rejareja na jumla katika matawi yake yote ya
Iringa, Pwani,Dodoma na Morogoro kwa shilling 500Tsh kwa chupa na katoni moja
kwa shilingi 5400.
END
TROPICAL FRESH JNUICE YAZINDULIWA RASMI:
Edited by Godfrey Mgallah.
Akizungumza na MOSJOSO blog msemaji mkuu wa kampuni
hiyo Hadija Said amesema kuwa “mbali na Tropical Fresh Juice kuwa na ladha
nzuri na yenye kumtamanisha mtumiaji kuitumia wakati wote pia inampatia
mtumiaji vitamin C pamoja na kumpa nguvu pindi anapotumia Juice hiyo”.
Hatahivyo msemaji huyo aliongeza kwa kusema bidhaa
hiyo ya Tropical Fresh Juice inapatikana kwa jumla na rejareja kwa matawi yote
ya kampuni ya Mambo Fresh Company kwa shilling 700/= kwa rejareja na shillingi
6500/= kwa jumla.
END
JUICE YENYE TIBA
YAGUNDULIKA:
Edited by Nasibu
Babisha.
ALOSERA ni juice
inayotengenezwa na kampuni ya CRA iliyopo Manispaa ya Morogoro juice hii
imedhibitiswa rasmi na mkemia mkuu wa kampuni hiyo .
Aidha mkemia huyo
ameongeza kwa kusema kuwa “juice hii sio
tu inatibu magonjwa bali upunguza kitambi, kuongeza damu na kuongeza vitamin C
na D mwilini.
END
0 comments:
Post a Comment