Habari Mpya

Saturday, July 29, 2017

Exim Bank yatembelea 'MSJ'

Benki ya Biashara ya Exim imepata nafasi ya kutembelea Chuo Cha Uandishi Wa Habari Morogoro 'MSJ' na kuongea na serikali ya wanafunzi chuoni hapo mwanzoni mwa wiki hii
Akiongea na wanafunzi hao meneja masoko wa Benki hio Oscar Awadh Mbode amesema Wameamua kuonga na wanafunzi ili kuona wanawezaje kuwasaidia katika mpango wao wa kufungua Akaunti ya wanafunzi ambacho kimekua kilio cha wanafunzi hao kwa muda mrefu
"Tumekuja kufanikisha suala lenu la akaunti,benki nyingi nchini zimekua na utaratibu mgumu wa kuanzisha akaunti za wanafunzi lakini sisi tumedhamiria kulimaliaza"alisema bwana Mbode
meneja wa masoko exim bank Oscar Mbode akitolea ufafnuzi jambo ofisini 'MOSJOSO'                                                                                                                                                                                                         

































Aidha Mbode ametoa faida watakazopata wanafunzi hao kwa kufungua akaunti ya exim
"Kwanza kufungua akaunti ni bure,mnachotakiwa kuleta ni barua tu kutoka katika uongozi wa chuo na serikali ya mtaa chuo chenu kinapopatikana,lakini fida nyingineni kuwekea asilimia tano za kiasi kilichopo  kila mwisho wa mwaka"alisema bwana Mbode
kwa niaba ya wanafunzi wa chuo hicho Rais wa chuo hicho Amani Christopher aliishukuru benki hio na kuahidi kushirikiana nao katika mchakato huo wa kufungua akauni ya wanafunzi chuoni hapo
Next
This is the most recent post.
Older Post
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: Exim Bank yatembelea 'MSJ' Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top