Makao makuu ya Umoja wa
Afrika, Addis Ababa,Ethiopia
Umoja wa Afrika umesema hautawapeleka
waangalizi wake wa uchaguzi katika uchaguzi wa wabunge wa Burundi utakaofanyika
Jumatatu kwa sababu masharti ya uchaguzi huru na wa haki hayajazingatiwa.
Vyama vya upinzani vimesusia uchaguzi wakipinga uamuzi wa Rais Pierre
Nkurunziza wa kugombea muhula wa tatu katika uchaguzi wa rais mwezi ujao.
Mapema Jumapili, Spika wa bunge la Burundi Pie Ntavyohanyuma alisema
alikimbia nchi yake kwa sababu ya kuhofia usalama wa maisha yake baada ya
kumshauri rais asigombee tena.
Jaribio la Bwana Nkurunziza kupata muhula wa tatu limekumbana na wimbi la
ghasia ambapo zaidi ya watu sabini wameuawa.
|
0 comments:
Post a Comment