Habari Mpya

Tuesday, March 10, 2015

Zitto Kabwe avuliwa rasmi uanachama Chadema

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe akifurahia jambo na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu walipokuwa kwenye kikao cha Bunge hivi karibuni . Picha na Mkataba
(Mwananchi news paper 11/3/2015)

Habari zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema), Tundu Lissu ametangaza kuvuliwa rasmi uanachama kwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe.

Baada ya Mahakama Kuu Tanzania kanda ya Dar es Salaam leo kutupilia mbali kesi iliyokuwa imefunguliwa na Zito Kabwe dhidi ya Chama Cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) ya kuhoji uhalali wa uanachama wake ndani ya chama hicho…

Habari zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo Tundu Lissu ametangaza kuvuliwa rasmi uanachama wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe.

Akitangaza hatua hiyo ya kumvua uanachama,Lissu amesema kanuni na sharia za chama hicho ziko wazi na zinaelekeza kuwa endapo mwanachama yeyote atakishtaki chama hicho mahakamani na iwapo atashindwa atakuwa amejiondoa mwenyewe kwenye chama
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: Zitto Kabwe avuliwa rasmi uanachama Chadema Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top