Habari Mpya

Monday, March 30, 2015

Wagombea urais Nigeria mchuano ni mkali




Huku nusu ya matokeo katika uchaguzi wa rais nchini Nigeria yakiwa yametangazwa, mgombea kutoka chama kikuu cha upinzani, Muhammadu Buhari, anaongoza dhidi ya rais aliye madarakani, Goodluck Jonathan.

Lakini majimbo ya kusini yenye idadi kubwa ya watu kama vile Lagos na Rivers bado hayajatangaza matokeo na mwandishi wa BBC mjini Abuja amesema mchuano bado ni mkali.

Tume ya uchaguzi imesema itaendelea kutangaza matokeo ya uchaguzi Jumanne asubuhi na kwamba matokeo ya mwisho yanatarajiwa kutolewa baadaye siku hiyo. Mwandishi wa BBC anasema yeyote atakayeshinda, litakuwa jambo la kushangaza iwapo mgombea atakayeshindwa hatatamka kuwepo kwa mbinu chafu.

(Bbc swahili)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: Wagombea urais Nigeria mchuano ni mkali Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top