Habari Mpya

Sunday, March 8, 2015

Simba ni moto mkali kwa yanga

Kocha mkuu wa Simba Goran Kopunivic (katikati)akimpongeza mshambuliaji Emmanueli okwi (kushoto)baaada ya kuifungia timu hiyo bao 1-0 dhidi ya watani wao wa jadi yanga katika mechi ya ligi kuu Tanzania bara iliyofanyika katika uwanja wa Taifa Dar es salaam jana kulia ni Simon Seerukuma.(picha na mtandao)



Timu ya Simba SC ya jijini Dar es Salaam, leo imeendeleza ubabe dhidi ya Yanga SC baada ya kuifunga goli 1-0 goli lililowekwa kimiani na mshambuliaji Emmanuel Okwi katika dakika ya 53 kipindi cha pili

Mechi hiyo ya ligi kuu imefanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ikuhudhuriwa na maelfu ya mashabiki kutoka katika pande zote za timu hizo waliofurika kwa wingi uwanjani.

Katika mchezo huo uliochezeswha na mwamuzi Martin Saanya wa Morogoro akisaidiwa na Souda Lila wa Dar pamoja na Florent Zablon wa Dodoma ulimalizika kwa kiongo wa Yanga Haruna Niyonzima kuzawadiwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: Simba ni moto mkali kwa yanga Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top