Alikuwa nahodha wa Ivory Coast
Yaya Toure aliyeanza kuwanyanyua mashabiki wa Ivory Coast alipofunga goli
katika dakika ya 20 kutokana na mkwaju mkali na kumwaacha mlinda mlago wa DR
Congo, Kidiaba, asijue la kufanya.
DR Congo wakasawazisha bao hilo
katika dakika ya 24 kwa njia ya penalti likifungwa na Mbokani Bezua.
Gervinho akafunga bao la pili
katika dakika ya 41. Hivyo hadi mapumziko Ivory Coast ilikuwa mbele kwa mabao
2-1.
Kipindi cha pili timu hizo
ziliendelea kushambuliana. Wilfried Kanon alikamilisha sherehe kwa timu yake ya
Ivory Coast alipofunga bao la tatu katika dakika ya 68. Kwa matokeo hayo Ivory
Coast imetinga fainali za michuano ya Afcon mwaka 2015, ambapo inamsubiri
mshindi wa nusu fainali ya pili, kati ya Ghana na wenyeji Equatorial Guinea, Alhamisi


0 comments:
Post a Comment