| mwanzo katika maandalizi kabla ya safari |
| maombi yakiongozwa na Naibu waziri wa ulinzi MSJOSO |
| TAYARI KWA KUONDOKA |
| wakaanza kuaga ndugu, jamaa, na marafiki mwanzo wa safari |
| katika kila jambo lenye Amani furaha utawala pasipokujali ni mkubwa au mdogo atajaribu kuonyesha furaha yake... na hivi ndivyo ilivyokuwa ndani ya gari wakati wa safari ikiendelea |
| spidi 120 |
| raha ya magari ya kukodisha... mda wowote mkitaka kuchimba dawa ruksa!!!! katikati ya safari RUVU |
| safari salama chini ya uongozi wa Coordinator of Studies |
| tukakafika Dar, salama... na kituo cha kwanza cha mafunzo... NEW HABARI COOPARATION |
| mwenyeji wetu akihakikisha tunatoka na jambo jipya kuhusu gazeti |
| wenyeji wakisaidiana kujibu maswali magumu toka kwa wana MSJ |
| tukapelekwa kitengo cha uandaaji wa habari za michezo..... |
| ndani ya production room, (LAYOUT) |
| mkuu wa kitengo cha ICT akijitaidi kujibu na kufafanua maswali ya wanachuo |
| tulimalizia ziara ya gazeti kwa kutembelea waandaji wa gazeti la THE AFRICAN humo full kingereza... ila maswali yakawa kama mvua... |
| KITUO CHA PILI, CLOUDS MEDIA, dada Joyce akijitaidi kujibu maswali yaliyokuwa yakija kwa mfululizo |
| ndani ya kitengo cha uandaaji wa vipindi vya video na matangazo... Clouds TV |
| ufafanuzi wa utumizi wa video Program tofautitofauti |
| maswali yalikuwa mengi kama watu wamejipanga namna ya kuuliza maswali.... |
| hapa ndipo sehemu ambayo panatengenezewa vipindi vya TV, kwa wanao angaliaga CLOUDs watapajua hapa |
| duh, ghafla akakatiza BABA JOHNiiii.... na kupigwa na swali la kichwa.. (kwanini anatumika kuharibu lugha ya kiswahi??? kwa kugeuza utamshi wa baadhi ya maneno kama... omeona BHANA! |
| ilimsumbua sana kujibu swali hilo... ila aliwezakutumia siasa flani kututuliza.. tukapoa kwasababu alikuwa anaingia kuendesha kipindi |
| waliokutana na rafiki zao tangu enzi ya kindagaten (chekechea) ikawa furaha sana |
| wataamu wakiwa bize kuonyesha namna ya wao wanavyoanda vipindi na kufanya mambo chroma |
| kila mmoja akisubiria kama atapata jibu la swali lake alilokuwa nalo kichwani mwake |
| mwisho wa siku tukamalizia ufukweni kuyaweka vizuri, mambo tuliyoyapata siku nzima,.... hapa Naibu Waziri waelimu kapata muda wa kupumzika.... |
| huu ni mwonekano wa bahari ya Hindi, katika mji wa Bagamoyo |
| waliojua kutumia maji ya bahari walionyesha ufundi wao... |
| hakuna aliyedhania kama huyu mrembo alikuwa anajua kuogelea... |
| wapo waliyoogelea na walioishia kuchezea maji... |
| mapozi ya kibaharini ndani ya nguo za ufukweni... |
| baada ya kutoka kuoga watu wakarefresh mind zao kwa kuburudika na muziki... kabla ya msosi wa jioni |
| chezea mduara wewe..... |
| kama utani watu wakaburudika kama wapo club... kumbe mziki wa SIMU |
| baada ya kuoga.... msosi wa jioni... full kujichagulia... SAMAKI, au KUKU, au NINI we sema utapewa... |
| wa chips kuku walikuwepo pia |
| asubuhi kukakuchwa... picha ya mahali tulipo jilaza usiku mzima |
| he! kwa watu.. kwa watu! ghafla gari likagoma kuwaka na siyo kawaida |
| sukuma wee..! lakini wapi.... |
| duh! ikabidi tuambizane kwa yeyote aliyechukua au kuokota chochote arudishe kimyakimya pale alipokichukua... |
| kuja kusukuma... kidogo tu! likawaka na safari ikaanza.. |
| katika makumbusho ya KAOLE... mwongozaji akitupa maelezo kwa ufupi... |
| wakusikiliza, kurekodi kwa simu nao walikuwa bize kweli... ili wasipitwe na kitu |
| wakuandika nao haoo... |
| wa taalamu wa video walijitaidi kwa hali na mali hawakosi tukio... |
| ziara ikaanzia katika kisima cha maajabu... watu bize kushuhudia... |
| soma kibao hichi |
| na hapa ndipo walipozikwa |
| kaburi la mtabiri |
| safari kwenda kuona mikoko... katika bandari ya kale ya Kaole.. |
| maelezo kuhusiana na kufa kwa bandari hiyo |
| soma, kuijua Kaole |
| kuwasili katika bwawa la mamba |
| maelezo kuhusiana na Mamba |
| kanisa lilipoingilia... maelezo kuhusiana na hapo |
| picha ya pamoja katika kumbukumbu hiyo ya kanisa lilipoingilia |
| wapo waliojua umuhimu wa sehemu hiyo... na kufanya maombi kwa imani |
| mbuyu uliopandwa na wahasisi wa kanisa la RC hapa TZ |
| mahali palipolazwa mwili wa living stone kutokea Zambia... kwa safari ya kwenda Uingereza kwa mazishi yake |
| jengo la kale la kanisa la RC... |
| waliotaka ukumbusho |
| safari ikafikia mwisho... kuwasili katika Chuo Cha Uandishi wa Habari Morogoro |
| watu wakiawa wanatawanyika makwao |
SHUKRANI ZIWAENDE MSJ STAFF, WIZARA YA ELIMU - MOSJOSO, na
WANAFUNZI WOOOTE WA MSJ 2013@

0 comments:
Post a Comment