Habari Mpya

Friday, May 3, 2013

UHURU WA VYOMBO VYA HABARI NI CHANGAMOTO


May 3, 2013,
Jakaya+Kikwete+Obama+Delivers+Address+Symposium+sfjZO4OTwTvl[1]

Na Claudia Kayombo

Wanahabari wa Jumuia ya Afrika Mashariki, wanaungana na wenzao duniani kuadhimisha siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari.
Miongoni mwa mambo ambayo yanatarajiwa kutawala wakati wa maadhimisho hayo ya siku tatu, ni majadiliano ya namna ya kuondoa utata wa mazingira ya waandishi wa habari kufanyia kazi hususan nchini Tanzania.
Maadhimisho hayo kwa ukanda huo, yanaadhimishwa mkoani Arusha Tanzania.
Hata hivyo wakati katika Jumuia ya Afrika Mashariki wawakishi wakikutana Arusha, kwa upande wao waandishi wengine wanayaadhimisha kwa kila mkoa kupitia klabu zao.
Wakati maadhimisho hayo yakifanyika, vichwa vya wanahabari nchini, vimebeba wasiwasi baada ya 
 miaka ya hivi karibuni kutokea matukio yanayotishia usalama wa maisha yao.

Mashaka katika vichwa vya waandishi yamekuja baada ya matukio mawili ya vifo vya waandishi na la tatu la kutekwa, kung’olewa jicho, meno kwa mmoja wa nguli wa tasnia hiyo, Absalom Kibanda.

Katika mazingira yanayoonesha kuwa, Kibanda pengine aliponzwa na ukali wa kalamu yake, ni pale aliposubiriwa katika geti la nyumba yake na kufanyiwa unyama huo.

Ukweli wa mambo ni kwamba maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya habari duniani yawe mwanzo wa kukoma kwa vitendo vya ukatili dhidi ya wanahabari nchini.

Pia iwe chachu kwa wamiliki wa vyombo vya habari kuwalipa waandishi wa habari mishara yao kwa wakati kwani hiyo ni changamoto ambayo sasa ipo katika ofisi nyingi za vyombo vya habari hivyo kuwafanya wageuke kuwa ombaomba au wasaliti wa fani hiyo

chanzo na Jambo Leo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: UHURU WA VYOMBO VYA HABARI NI CHANGAMOTO Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top