Neno ‘uhuru’ linamaanisha ni hali ya kujitawala na kujiamulia
kupanga na kutekeleza katika hali isiyo na shuruti pasipo kuvunja
sheria na kanuni.
Tarehe 3 mei ya kila mwaka ni siku ya uhuru wa vyombo vya habari
Duniani. Kama ilivyo ada mwaka huu pia Tuzo hizo za Umahiri wa Uandishi
wa Habari Tanzania (EJAT) ziliandaliwa na Baraza la Habari Tanzania
(MCT) na kutolewa katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi.
Waandishi wengi waliibuka na tuzo hizo. Kwangu ninazichukulia tuzo hizo
kuwa ni changamoto kubwa kwa waliozipata na wasiozipata. Kwa waliopata
tuzo tuzo hizo wasibweteke kwa kuwa wametuzwa bali watambue umuhimu wao
katika kusaidia jamii katika kuibua kero mbali mbali katika jamii yetu
ambazo ni kiwazo cha maendeleo.
Kwa waandishi ambao hawakupata tuzo ni budi wakaongeza bidii
katika kuandika habari zenye msukumo wa maendeleo na zenye tija kwa
jamii. Japo habari za kijamii ambazo zinaibua kero muhimu katika jamii
nyingi kati ya hizo hupatikana vijijini ambako vyombo vyetu vingi vya
habari situ havifiki huko bali vyombo vya habari huwa haviwawezeshi
waandishi kwenda vijijini kufanya tafiti na kuibuka na habari hizo
Lakini pia ifahamike kuwa kutokana na
matakwa na maelekezo ya wamiliki walio wengi habari za kijamii hazina
nafasi na haziuzi.Wamiliki wa vyombo vingi vya habari huegemea na kutoa
maelekezo kwa wahahariri kuandika habari za kisiasa kwani ndizo
huonekena kuwa zina soko na faida nyinginezo hasa mahusiano kati ya
wamiliki na watawala.
Ni kawaida yangu kutafakari kwa kina masuala mbali mbali ya kisiasa
na kijamii . Nimejijengea mazoea ya kuzama kwa kina kuangalia changamoto
mbali mbali zinazokabili jamii ya Kitanzania, Afrika na Ulimwengu kwa
ujumla. Kutokana na mazoea hayo ndipo ninapojikuta ninatafakar kwa kina
juu ya siku hii adhimu kwa waandishi wa habari. Siku ya uhuru wa vyombo
vya habari.
Kama jina la siku linavyojieleza, ‘siku ya uhuru wa vyombo vya
habari’. Kabla ya kwenda mbali zaidi yapo maswali ya kujiuliza. Ni
uhuru wa vyombo vya habari au uhuru wa waandishi wa habari? Na je chombo
cha habari chaweza kuhesabika kuwa huru pasipo mwandishi kuwa huru?
Kulingana na hali ilivyo hususani hapa kwetu Tanzania ni yupi mwandishi/
chombo kilicho huru? Na mwisho tujiulize swali hili ni uhuru wa
waandishi wa habari/vyombo vy habari au wamiliki wa vyombo hivyo na
maswahiba zao wanasiasa?
Hapa kwetu Tanzania tunavyo vyombo vingi sana vya habari. Je
viko huru? Tunavitambuaje vyombo vya habari vilivyo huru? Na kwa uapnde
wa waandishi wa habari, je ni changamoto zipi zinazowakabili? Wanafanya
nini kuzitatua? Hawajafungwa katika minyororo ya dhuruma na manyanyaso
ya wamiliki na wanasiasa? Hii ni mada ndefu. Nionavyo ni kama vile
uhuru kama wa waandishi waa habari haujapatikana. Uhuru uliopo ambao
unahesabiwa kuwa ni uhuru wa vyombo vya habari upo kwa wamiliki wa
vyombo vya habari. Kwani hawa wengi wao huamua nini kiandikwe/kitangazwe
katika vyombo vyao hususani vyombo vinavyomilikiwa na watu bianafsi.
Kwa upande wa vyombo vinavyomilikiwa na Serikali matakwa ya Serikali
(watawala) ndio hutawala katika uendeshwaji wa vyombo hivi. Ijapokuwa
vyombo hivi vya serikali huendeshwa na kodi za wananchi lakini hugeuka
kuwa vyombo vya propaganda vya serikali. Na tujiulize ni mara ngapi
vyombo hivi vya umma vimekejeli vyama vya siasa? Je ni mara gapi vyombo
hivi vya umma vimelalamikiwa kupendelea chama tawala hususani wakati wa
uchaguzi?
Vyombo vya habari vya binafsi na vya serikali mara nyingi
vimelaumiwa kwa kuendesha propaganda zisizo na tija kwa lengo la
kumneemesha mtu au kundi fulani.
Sisi waaandishi wa habari wengi wetu tumeacha taaluma zetu
zinazoelekeza miiko ya uandishi wa habari. Tumekubali kutumiwa mithiri
ya kwa muda mfupi na watu binafsi,wanasiasa na makundi mengene ya
kijamii kwa binafsi na kasha kuachwa/kutupwa mithili ya kondom ilikwisha
tumika. Licha ya umuhimu mkubwa wa waandishi wa habari katika
kufanikisha kampeni za kijamaii lakini mchango wao hauthaminiki sit u na
watawala bali hata jamii kwa ujumla wake.
Wamiliki wa Vyombo vya habari wamekuwa ni miungu watu. Manyanyaso
visa na mikasa ni sehemu ya adha azipatizo mwandishi wa habari wa
Tanzania.
Licha ya waandishi kulipwa ujira mdogo mno usiokidhi mahitaji
vyombo vingi vya habari haviwalipi waandishi kwa wakati. Mishahara yao
imekuwa ikichelewa mno na kuna wakati hawalipwi kabisa. Hii huwapelekea
waandishi kuishi kwa bahati nasibu. Hapo ndipo umahiri wa kazi hupungua
na ndipo mwandishi huacha kufuata miiko ya uandishi wa habari na
kujitumbukiza katika vitendo vya rushwa na aina nyingine ya ufisadi.
Maisha ya mwandishi wa Tanzania anayeadhimisha uhuru wake ifikapo tarehe 3 may ya kila mwaka yapo mashakani.
Waandishi wengi wanaishi kama omba omba. Kwenye mikutano ya
waandishi wa Habari (Press Comference) ni eneo ambalo waandishi
huadhirika na kudharirika. Bahasha ndio mkombozi wao
. Baadhi ya waandaaji wa mikutano hii huwanyanyasa waandishi mithiri ya
watumwa. Kazi bado na safari ya uhuru kamili ya uandishi ni ndefu.
Sheria ya habari ya mwaka 1976 ni kikwazo kingine kwa uhuru kamaili wa
uandishi wa Habari na vyombo vya habari. Kuna kila sababu ya kuitazama
upya sheria hii. Wamiliki wa vyombo vya habari na wanasiasa ni kiwazo
kikubwa kwa uhuru wa waandishi wa habari na ustawi wa taaluma ya
uandishi wa Habari Tanzania. Mwisho nimalize kwa kutoa waito kuwa ni
vema uhuru wa vyombo vya habari ukatazamwa upya kulingana na changamoto
zinazokabili tansinia ya habari Tanzania.
Wednesday, April 17, 2013
- Blogger Comments
- Facebook Comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment